TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tarehe 15 Januari, 2024 – No. 001/01/2024

Chama cha Movement for the Republic and Democracy (MRD) kinasikitishwa sana na kuzorota kwa hali ya kisiasa na kiusalama katika ukanda la Maziwa  Makuu pamoja na hali ya taharuki kufuatia uchokozi wa Rwanda dhidi ya jirani yake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande moja; na kwa upande nyingine , chokochoko zisizokoma za Rwanda dhidi ya Burundi.

Licha ya juhudi za watendaji mbalimbali la ukanda na jumuiya la Umoja wa  kimataifa, kwa kurejesha amani na utulivu, utawala wa Paul Kagame unaendelea na vita vyake vya unyakuaji na uporaji wa rasilimali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pamoja na kuvunja utulivu wa nchi nyingine jirani ikiwemo taifa la Burundi chini la mwavuli la vikundi vya kigaidi kama vile M23 na RED TABARA.

Tunatoa wito kwa wananchi wote wa Rwanda kulaani, kwa sauti moja, utawala na itikadi kali wa RPF pamoja na kiongozi wake, dhalimu Paul Kagame, wakati wakisimama kwa mshikamano pamoja na wananchi ndugu wa Kongo na Burundi.

Tunataka jeshi la Rwanda liondolewe mara moja na bila mashariti yeyote katika maeneo yote ya Kongo na kukomesha mara moja uungaji mkono wa Rwanda kwa vikundi vya kigaidi vya M23 na RED TABARA.

MRD inatoa wito kwa kurejeshwa  mara moja bila mashariti yeyote huko nchini Burundi, ikifanywa na Rwanda; wahusika wa jaribio la mapinduzi ya mwaka 2015, wanaoendelea kutekeleza uhalifu na ugaidi katika ardhi ya Burundi, ili kuweza kupata fursa ya maelewano mazuri kati ya nchi hizo mbili ndugu.

Tunapongeza juhudi za amani za viongozi wa nchi za kanda hii kwa ujumla na hasa wa jumuia la SADC.

Hatimaye, tunatoa wito kwa Wanajamhuri na Wanademokrasia wote wa Rwanda kuchanganya juhudi zetu na kufanya kila iwezekanalo ili kukomesha utawala wa jinai wa RPF, na kurejesha amani pia utulivu katika ukanda la maziwa makuu.

Washington DC,  Januari 15, 2024

Mama Christine Coleman

Rais wa MRD

Be the first to comment

Leave a Reply